katiba_viwawa2010


 

KATIBA YA VIWAWA: 2010

YALIYOMO                                                                                                           

i    Vifupisho

ii    Utangulizi

  1. Maana ya Viwawa
  2. Anwani ya Chama
  3.  Ofisi ya chama
  4. Dira ya Viwawa
  5. Utume wa Viwawa
  6. Malengo ya Viwawa
  7. Uanachama
  8. Muundo wa Chama
  9. Uongozi wa Chama
  10. Mikutano
  11. Wajumbe wa Mikutano ya Viwawa
  12. Majukumu ya Kamati
  13. Mapato ya chama
  14. Kamati ndogondogo
  15. Muhimu
  16. Mengineyo

 

 

 

 

                 i. TAFSIRI YA VIFUPISHO

 

o   KAMATI   - Kamati Tendaji

o   VIWAWA -  Vijana Wakatoliki Wafanyakazi

o   TYCW - Tanzania Young Catholic workers.

o   TEC - Tanzania Episcopal Conference.

o   ICYCW  – International Coordination of Young Christian Workers.

o   YCS – Young Catholic Students

o   OFM – Ordo Fratrum Minorum

 


ii.  UTANGULIZI

HISTORIA YA VIWAWA TANZANIA:

VIWAWA ilianzishwa mwaka 1924 mji wa Brussel nchini Ubelgiji na Kadinali Joseph  Cardjin nakupitishwa rasmi kama Chama cha Kitume cha Vijana Kimataifa na Baraza la Kipapa Vatcan mwaka 1950.Kadinali Joseph Cardjin pia alianzisha YCS,hivyo VIWAWA na YCS alianzisha yeye.

 

Makao Makuu ya Viwawa Duniani Yako Roma – Italia. 

Viwawa iliingia Tanzania mwaka 1959 katika Parokia ya Msimbazi, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, chini ya Mwanzilishi Pd. Lucas Gaemperle OFM,  badaye mwaka 1960 alifika nchini kwetu Pd. Hendrikus Johannes Brinkhof maarufu kama Pd Mansuetus ambaye alimsaidia kwa karibu sana, padri Lucas kuueneza utume wa viwawa nchini kwetu, na kufuatiwa na Parokia ya  St. Joseph, Kurasini, Magomeni, Chang’ombe, Kibaha.

 

Mwanzilishi wa viwawa duniani Kardinali Joseph Cardijn alitembelea Tanzania, jimbo la Dar es salaam tarehe 17 – 6 – 1960.

 

Padri Lucas   Gaemperle OFM ambaye alikuwa mwanzilishi wake alitembea sehemu nyingi za Afrika na Ulaya kwa lengo  la kujifunza utume huu.  Mwaka 1961 VIWAWA Tanzania walitembelewa na mjumbe kutoka Makao Makuu Roma Italia na alitembelea matawi ya Dar es Salaam na Moshi.  Mjumbe huyo alifanyakazi ya kuunganisha utume huu hapa Tanzania na huko Zambia.  Mwezi Novemba 1964 Kamati kuu ya VIWAWA ulimwenguni walifanya mkutano hapa Tanzania, Mkutano huu ulifuatiwa na ziara za mafunzo ili kuona maendeleo ya Viwawa hapa Tanzania.  

 

Mnamo mwaka 1966 Viwawa walifanya mkutano mkuu wa kitaifa na ni majimbo mawili tu ndiyo yalihudhuria Dar es Salaam na Moshi yakiwakilishwa na wajumbe kumi na mmoja.  Mwaka 1973 mkutano mkuu ulifanyika jimboni Iringa na ndipo kwa mara ya kwanza katiba ya Viwawa iliundwa, na kupitishwa rasmi kama chama cha kitume cha vijana na Baraza la Maaskofu katoliki Tanzania (TEC) mwaka 1979. Mshauri wa kwanza wa viwawa Taifa Padri Pius Shayo aliyeteuliwa katika mkutano mkuu wa baraza la maaskofu Tanzania uliofanyika tarehe 23 – 27 October, 1979.

 

Baada ya kupitishwa hapo kilitambulika pote Tanzania kama Chama cha Vijana Wakatoliki Wafanyakazi Tanzania (VIWAWA)Mpaka sasa, chama hiki kipo majimboni, kuanzia ngazi ya Jumuiya, Mtaa, Kanda, Kigango, Parokia, Jimbo, Taifa na Kimataifa.

 

 


 


1.0  MAANA YA VIWAWA

 

1.1  VIWAWA ni chama cha kitume cha Vijana Wakatoliki Wafanyakazi ambao wanatumwa na Kanisa ili kueneza habari njema ya kwamba Yesu Kristu ndiye njia ya ukweli na uzima kwa vijana wote katika maisha yao ya kila siku.

 

1.2   Wafanyakazi: Ni vijana wa wanaume na wanawake waishio mijini, vijijini na walio kwenye masomo, mafunzo ya fani mbalimbali, walio katika ajira rasmi na zisizo rasmi.

 

1.3  Viwawa ni chama ambacho kinawaunganisha vijana na kuwasaidia waone hali yao, kuamua juu yake katika mwanga wa Injili na kuwaongoza kufanya matendo ya kubadilisha hali zao na kutengeneza ziwe nzuri zaidi kwa njia ya Tafakari ya Maisha.

Chama hiki huongozwa na vijana wenyewe katika ngazi zote na huwa na Mshauri na Mlezi kwa ngazi ya Parokia,Jimbo na Taifa.

 

 

2.0  ANWANI YA CHAMA:

Vijana Wakatoliki Wafanyakazi.

S.L.P 2133, DAR ES SALAAM - TANZANIA.

 


 

3.0  OFISI ZA VIWAWA.

3.1  Ofisi ya viwawa taifa itakua pale yalipo makao makuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania.(TEC)

3.2  Ofisi ya jimbo itakua pale yalipo makao Makuu ya Jimbo.

3.3  Ofisi ya parokia itakua parokiani. 

    

4.0  DIRA YA VIWAWA

Kumwona Kijana Mkatoliki Mfanyakazi anayejimudu katika maisha yake ya kimwili na kiroho kwa kutumia njia ya Tafakari ya Maisha.

 

5.0  UTUME WA VIWAWA

Kumwezesha kijana kuwa Mkristo wa kweli ambaye ana ujasiri wa kurekibisha,

kuendeleza na kudumisha taratibu za utamaduni, uchumi, siasa na

utaalamu kufuatana na mpango wa Mungu.

 

6.0  MALENGO YA VIWAWA

6.1  Kuwawezesha Vijana kutambua wajibu wao katika kujielimisha na kujitegemea katika maisha yao.

6.2  Kustawisha na kusaidia Kanisa kwa kushiriki katika kazi za Kanisa, kuhusu maendeleo ya Kiroho, Kimwili, Kiakili na Kijamii.

6.3  Kutangaza habari za Kanisa na kujaribu kwa kila hali kuleta uhusiano mwema baina ya vyama vya kitume,madhehebu mbalimbali na dini nyingine.

6.4  Kuchukua hatua za kufaa kuendeleza mambo yote yanayoonekana kwamba ni ya manufaa kwa Kanisa na Ustawi wa jamii.

6.5  Kuwajenga vijana katika mazingira ya kuwa na mwenendo mwema kwa kanuni ya Tafakari ya Maisha inayoongozwa na mtindo wa Kuona-Kuamua na Kutenda. Na mitindo mingine ya malezi inayofaa.

6.6  Kuwakumbusha vijana wote kwamba sote tunategemeana kwa kushauriana, kuongozana na kufundishana kimwili na kiroho.

7.0  UANACHAMA:

Kuna aina tatu za uanachama.

7.1  Wanachama washiriki

7.1.1        Awe kijana Mkatoliki mwenye umri kati ya miaka 14 hadi 17.

 

7.2  Wanachama kamili

7.2.1        Kijana Mkatoliki  mwenye Ubatizo.

7.2.2        Awe na umri kati ya miaka 18 hadi 35.

7.2.3        Awe mwenye Akili timamu.

7.2.4        Awe na Mapenzi na VIWAWA..

7.2.5        Vijana ambao wameowa na kuolewa pia wanaweza kuwa wanachama na viongozi.

 

7.3  Wanachama maalumu

7.3.1        Aliyekwisha kuwa mwanachama kamili.

7.3.2        Watu wa wazima wenye mapenzi mema na chama.

 

7.4  Wajibu wa Mwanachama.

7.4.1        Kukubali kuongozwa na Mwongozo wa chama na kutekeleza malengo yake.

7.4.2        Kushiriki mikutano ya chama kwa mujibu wa KATIBA.

7.4.3        Kushiriki shughuli zote za VIWAWA.

7.4.4        Kushiriki katika chaguzi mbalimbali za VIWAWA.

7.4.5        Kulipa ada na michango maalum kwa wakati unaotakiwa.

7.4.6        Kuunga mkono na kusaidia kwa vitendo maendeleo ya VIWAWA.

             7.4.7     Kusikiliza na kufuata maelekezo mbalimbali ya Uongozi.

 

7.5  Haki za Mwanachama

7.5.1        Anahaki ya kuchagua au kuchaguliwa kwa mujibu wa ibara namba (7.1,2) na (9.2).

7.5.2        Kuchangia hoja na kusikilizwa katika mikutano kwa nidhamu

7.5.3        Kushiriki shughuli zote za VIWAWA kwa mujibu wa KATIBA.

7.5.4        Anahaki ya kupata huduma, faida zitokanazo na chama kwa mujibu wa taratibu za chama mahalia.

7.5.5        Mwanachama maalumu hawezi kuchagua au kuchaguliwa katika Uongozi.

7.5.6        Mwanachama maalumu hawezi kufanya maamuzi kwa niaba ya Kamati Tendaji

7.5.7        Mwanachama anapotuhumiwa anahaki ya kupewa fursa za kujieleza,kujitetea.

 

7.6  Ukomo wa Uanachama

7.6.1        Akikiuka maadili ya chama kama kushiriki katika kuihujumu VIWAWA

7.6.2        Kufariki dunia.

7.6.3        Kuvuka kikomo cha umri wa miaka 35.

7.6.4        Hiari ya mwanachama ambayo itadhibitishwa na Uongozi.

 

8.0   MUUNDO WA CHAMA.

        Kutakuwa na Ngazi Sita zaViwawa

8.1 Ngazi ya Jumuiya Ndogondogo

            8.2 Ngazi ya Kigango,Kanda.

             8.3 Ngazi ya Parokia.

             8.4 Ngazi ya Jimbo.

             8.5 Ngazi ya Taifa.

             8.6 Ngazi ya Kimataifa.

 

 

9.0  UONGOZI WA CHAMA.

9.1  Ngazi za uongozi

9.1.1        Mwenyekiti

9.1.2        Makamu wa Mwenyekiti

9.1.3        Katibu

9.1.4        Katibu Msaidizi

9.1.5        Mhazini

9.1.6        Mhazini Msaidizi

9.1.7        Mratibu (ngazi ya Jimbo na Taifa)

9.1.8        Wajumbe wa kuteuliwa wasio zidi wa tatu.

9.1.9        Mshauri

 

9.2  Sifa za uongozi

9.2.1        Kijana Mkatoliki

9.2.2        Asiwe na kizuizi chochote cha Sakramenti.

9.2.3        Mwenye umri kuanzia miaka 18 hadi 35.

9.2.4        Awe na Akili timamu

9.2.5        Uwezo na kipaji cha kuongoza, busara na hekima.

9.2.6        Awe na mapenzi na Viwawa

9.2.7        Kwa nafasi ya katibu awe na uwezo wa kusoma na kuandika vizuri.

9.2.8        Kwa nafasi ya Mhazini awe Mwaminifu, na kwa ngazi ya Parokia, Jimbo na Taifa awe na Ujuzi au Uzoefu wa maswala ya Fedha.

9.2.9        Kiongozi katika ngazi ya Jimbo na Taifa lazima awe na sifa za ziada kama uzoefu wa uongozi walau mwaka mmoja na kiwango cha elimu walau kidato cha nne au elimu inayolingana na hiyo.

 

9.3  Uchaguzi wa Viongozi

9.3.1        Viongozi watachaguliwa na mkutano mkuu baada ya miaka mitatu. 

9.3.2        Kiongozi anaweza kuchaguliwa vipindi vitatu mfululizo kama ataonekana  anafaa.

9.3.3        Uchaguzi utafuata taratibu zote za uchaguzi kama zilivyoainishwa kwenye katiba     ya Halmashauri ya Walei.

9.3.4        Wajumbe watakaoruhusiwa kupiga au kupigiwa kura ngazi ya taifa ni viongozi wa ngazi ya jimbo, kwa ngazi ya jimbo ni viongozi wa parokia, na kwa ngazi ya parokia ni viongozi wa kigango,kanda au jumuiya.

9.3.5        Viongozi wa Kamati Tendaji iliyomaliza muda wake  ni wajumbe halali wa kupiga na kupigiwa kura kwa kuzingatia ibara namba (7.2).

9.3.6        Mjumbe asiyekuwepo katika kikao cha uchaguzi kwa udhuru anaweza kuchaguliwa kama anasifa toshelezi za kiongozi.

9.3.7        Viongozi wakuu watatu watoke karibu na ofisi ya ngazi husika ili kuleta ufanisi wa kazi za Utume hasa kwa nafasi ya Mhazini.

9.3.8        Uchaguzi ngazi ya jumuiya, kanda, kigango utasimamiwa na viongozi wa viwawa ngazi ya parokia. Uchaguzi ngazi ya parokia utasimamiwa na viongozi wa viwawa jimbo husika, ngazi ya jimbo utasimamiwa na viongozi Viwawa ngazi ya Taifa ngazi ya Taifa utasimamiwa na Idara ya Walei TEC.

            9.4 Upigaji Kura

9.4.1    Kura zote ni lazima zifanyike kwa njia ya siri, kiongozi anayechaguliwa lazima apate zaidi ya nusu ya kura zote. Kama zikilingana mara mbili Msimamizi wa uchaguzi atakuwa na uwamuzi wa mwisho.Viongozi wapya watadhibitishwa na Uongozi wa Kanisa ngazi husika.

 

 

9.5 Mshauri,Mlezi wa chama

               9.5.1       Mshauri wa Taifa atateuliwa na Baraza la Maaskofu

         9.5.2       Mshauri wa Jimbo atateuliwa na Mkuu wa Jimbo

9.5.3           Mshauri wa Parokia atateuliwa na Paroko.

 

9.6      Wajibu wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti

9.6.1        Atakuwa kiongozi na Msemaji Mkuu wa VIWAWA.

9.6.2        Atasimamia mikutano ya kamati  tendaji na mikutano ya VIWAWA.

9.6.3        Asaidie na kuangalia kwamba viongozi wengine wote wanafanyakazi zao ipasavyo.

9.6.4        Kuona kuwa kila mjumbe anapata nafasi ya kutoa maoni yake katika mikutano.

9.6.5        Agawanye kazi na madaraka mengine kwa viongozi wenzake wa kamati ili asifanye kazi peke yake.

9.6.6        Atakuwa na kura ya uamuzi endapo kutatokea sare katika kura.

9.6.7        Atawajibika kwa kamati tendaji.

 

9.7      Wajibu wa Katibu na Katibu Msaidizi

9.7.1        Atakuwa Mtendaji wa VIWAWA.

9.7.2        Atatunza kumbukumbu zote za Mikutano.

9.7.3        Ataandaa agenda na dondoo za vikao

9.7.4        Atatoa taarifa zote kwenye Mkutano Mkuu wa Mwaka kuhusu maendeleo ya chama, katika kipindi kilichopita.

9.7.5        Kutayarisha na kuitisha mikutano yote ya chama akishauriana na Mwenyekiti.

9.7.6        Kupokea na kuzishughulikia ipasavyo barua zote zinazohusu Chama.

9.7.7        Atawajibika kwa kamati tendaji

 

9.8      Wajibu wa Mhazini na Mhazini Msaidizi

9.8.1        Kutunza fedha za chama sehemu salama Benki. Pia kuona kuwa  zinatumiwa kwa njia inayofaa.

9.8.2        Kuweka vitabu vya fedha kwa uangalifu.

9.8.3        Atatoa taarifa zote za fedha kwenye mikutano yote halali ya chama.

9.8.4        Kutayarisha makisio ya mapato na Matumiza ya fedha za Chama na kuwasilisha mbele ya kamati ya utekelezaji ili yathibitishwe.

9.8.5        Atatoa kumbukumbu zote za fedha kila itakapohitajika.

9.8.6        Kuhimiza na kupanga njia za kupata fedha za chama na kuona kwamba malipo yanafanywa kwa kadiri ya mapato na matumizi yaliyokubaliwa na chama – akishirikiana na Kamati Tendaji.

9.8.7        Atawajibika kwa kamati tendaji

 

9.9      Wajibu wa Mshauri,Mlezi

9.9.1        Kutoa mashauri ya Kiroho na ya shughuli za maendeleo katika chama.

9.9.2        Kuhudhuria Mikutano yote ya chama

9.9.3        Kuwa Mjumbe wa hadhi bila kuwa na kura.

9.9.4        Kudumisha na uhusiano mwema kati ya viongozi na wanachama kwa ujumla.

 

9.10   Kuacha au Kuachishwa Uongozi

9.10.1    Kushindwa kuhudhuria mikutano mitatu mfululizo bila taarifa maalum.

9.10.2    Kukiuka maadili ya uongozi.

9.10.3    Kwa kutoa taarifa ya maandishi kwa viongozi waliopo mwezi mmoja kabla.

9.10.4    Kutokana na sababu zisizo epukika.

9.10.5    Iwapo Kiongozi wa ngazi ya chini atateuliwa au kuchaguliwa kushika Nafasi ya ngazi ya juu ya Viwawa katika nafasi ileile Atajiuzulu na Atabaki kuwa mjumbe wa Kamati Tendaji wa ngazi ile aliyojiuzulu.

9.10.6    Nafasi iliyoachwa wazi kwa sababu yoyote ile, kiongozi wa muda atateuliwa na Kamati Tendaji kushika madaraka mpaka uchaguzi mwingine.

9.10.7    Ikiwa zaidi ya nusu viongozi wamejiuzulu uchaguzi utaitishwa upya kwa nafasi zote.

 

10.0          MIKUTANO

                Kutakuwa na Mikutano ifuatayo ya VIWAWA

10.1          Kamati ya Utendaji


10.1.1    Kamati Tendaji ngazi ya Taifa,itakutana kila baada ya miezi mitatu (mara nne kwa mwaka). Ngazi ya Jimbo kila baada ya miezi miwili (mara sita kwa mwaka) ngazi ya parokia,kigango na kanda mara moja kwa mwezi.

10.1.2    Kikao cha dharura cha Kamati tendaji kinaweza kuitishwa endapo kuna haja na ulazima wa kufanya hivyo.

10.1.3    Kikao cha Kamati Tendaji kitaitishwa na Katibu kwa kushauriana na Mwenyekiti.

10.1.4    Wajumbe wasiopungua nusu ya wajumbe wote wa Kamati ya Utendaji wanaweza kuitisha kikao kwa maandishi.

10.1.5    Taarifa ya kikao cha Kamati  Tendaji itatolewa kwa wajumbe siyo chini ya siku kumi kabla ya kikao.

10.1.6    Endapo idadi ya wajumbe waliohudhuria haifikii nusu ya wajumbe wa Mkutano, mkutano utahairishwa.

  

10.2          Halmashauri ya Utekelezaji


10.2.1    Itakutana mara moja kwa mwaka Taifa, Jimbo mara tatu, Parokia mara nne. 

10.2.2    Kuitisha Kikao cha dharura cha Halmashauri endapo kuna haja na ulazima wa kufanya hivyo.

10.2.3    Kikao cha Halmashauri kitaitishwa na Katibu kwa kushauriana na Mwenyekiti...

10.2.4    Wajumbe wasiopungua theluthi moja ya wajumbe wote wa Halmashauri wenye haki ya kuhudhuria wanaweza kuomba kimaandishi kuitishwa kwa kikao cha Halmashauri.

10.2.5    Taarifa za kikao cha Halmashauri itatolewa kwa wajumbe siyo chini ya siku thelathini kabla ya kikao.

10.2.6    Endapo idadi ya wajumbe waliohudhuria haifikii nusu ya wajumbe wa Mkutano, mkutano utahairishwa kwa muda usiopungua miezi miwili. Lakini endapo mahudhurio ya wajumbe hao ni zaidi ya theluthi moja ya idadi ya wajumbe wote wa Mkutano basi mkutano utafanyika.

 

10.3          Mkutano Mkuu


10.3.1    Ndicho kikao cha juu kuliko vyote vya VIWAWA.  Utaitishwa mara moja kwa mwaka Taifa, Jimbo mara mbili, Parokia mara tatu. Kigango na kanda mara nne.

10.3.2    Mkutano Mkuu wa dharura utaitishwa endapo kuna haja na ulazima wa kufanya hivyo.

10.3.3    Mkutano Mkuu utaitishwa na Katibu kwa kushauriana na Mwenyekiti wa ngazi husika.  Kamati tendaji inaweza, kwa maombi kimaandishi, ya wajumbe wasiopungua theluthi moja ya wajumbe wote.  Kuitisha kikao cha Mkutano Mkuu ikiona kuna haja na ulazima wa kufanya hivyo.

10.3.4     Taarifa ya kikao cha Mkutano Mkuu itatolewa kwa wajumbe siyo chini ya miezi miwili kabla ya kikao kwa taifa na mwezi mmoja kwa jimbo.

10.3.5     Endapo idadi ya wajumbe waliohudhuria haifikii nusu ya wajumbe wa Mkutano, mkutano  utahairishwa kwa muda usiopungua miezi miwili. Lakini endapo mahudhurio ya wajumbe hao ni zaidi ya theluthi moja ya idadi ya wajumbe wote wa Mkutano basi mkutano utafanyika.

 

11.0          WAJUMBE WA MIKUTANO YA VIWAWA

 

11.1          TAIFA

 

                        11.1.1    Kamati Tendaji ya Taifa

 

11.1.2 Halmashauri ya Utekelezaji Taifa

                                    11.1.2.1 Kamati Tendaji

                                    11.1.2.2 Mwenyekiti wa kila Jimbo.

                                    11.1.2.3 Mshauri kila Jimbo.

                       

                        11.1.3 Mkutano Mkuu wa VIWAWA.

                                    11.1.3.1 Kamati Tendaji ya Taifa.

                                    11.1.3.2 Mwenyekiti, Katibu na Mhazini kila Jimbo

                                    11.1.3.3 Mshauri,Mlezi wa Kila Jimbo

                                    11.1.3.4 Mshauri wa Viwawa  Taifa.

                                    11.1.3.5 Wajumbe maalumu (Waalikwa) Ikiwa lazima.

 

11.2 KIJIMBO:

                        11.2.1 Kamati Tendaji ya Jimbo

 

                        11.2.2 Halmashauri ya Utekelezaji ya Jimbo.

11.2.2.1Kamati Tendaji ya Jimbo

11.2.2.2Mwenyekiti wa kila Parokia.

11.2.2.3Mshauri wa kila Parokia.

11.2.2.4Mshauri wa Jimbo

 

                        11.2.3 Mkutano Mkuu wa VIWAWA.

                                    11.2.3.1 Kamati Tendaji ya Jimbo

                                    11.2.3.2 Mwenyekiti, Katibu na Mhazini wa kila Parokia

                                    11.2.3.3 Mshauri,Mlezi Jimbo.

11.2.3.4 Mshauri,Mlezi kila Parokia

11.2.3.5 Wajumbe maalumu (Waalikwa) Ikiwa lazima.

 

11.3 KIPAROKIA

 

                        11.3.1 Kamati Tendaji Parokia

                       

                        1.3.2 Halmashauri ya Utekelezaji Parokia

                                    11.3.2.1 Kamati Tendaji

                                    11.3.2.2 Mwenyekiti wa kila Kigango,Kanda,Jumuiya.

                                    11.3.2.3 Mshauri Parokia

 

 

11.3.3.0 Mkutano Mkuu wa VIWAWA

                                    11.3.3.1 Kamati ya Utendaji ya Parokia

                                    11.3.3.2 Mwenyekiti, Katibu na Mhazini kila Kigango,Kanda,Jumuiya.

                                    11.3.3.3 Mshauri,Mlezi wa Parokia..

11.3.3.4Wajumbe maalumu.(waalikwa) Ikiwa lazima.

            

 

 

 

 

 

 11.4.0  KIGANGO, KANDA

11.4.1 Kamati Tendaji ya Kigango,Kanda.

 

11.4.2.Halmashauri ya Utekelezaji ya Kigango,Kanda

             11.4.3 Kamati Tendaji

             11.4.4 Mwenyekiti,Katibu na Mhazini kila Mtaa,Jumuiya.

             11.4.5 Mshauri,Mlezi Kigango,Kanda.

 

                        11.5.5 Mkutano Mkuu

                                    11.5.5.1 Kamati Tendaji ya Kigango,Kanda.

                                    11.5.5.2           Wanachama wote wa Kigango,Kanda,Jumuiya.

                                    11.5.5.3 Mshauri,Mlezi wa Kigango,Kanda.

 

12.0 MAJUKUMU YA KAMATI

 

12.1 Majukumu ya Kamati Tendaji (Kigango, Parokia, Jimbo na Taifa)

12.1.1    Kuhakikisha kuwa maazimio ya chama yanatekelezwa

12.1.2    Kutayarisha hija, Semina, Mafungo na Mikutano ya Chama.

12.1.3    Kudumisha uhusiano na vyama vingine ndani na nje ya Kanisa.

12.1.4    Kutayarisha na kupanga miradi mbalimbali kwa jumla.

12.1.5    Kuteua kiongozi atakayeshika nafasi yoyote iliyo wazi hadi uchaguzi mkuu.

12.1.6    Kuteuwa wajumbe wa Kamati Tendaji na Kamati ndogondogo za Chama.

12.1.7    Kutayarisha Kalenda ya Matukio ya Mwaka.

12.1.8    Kuhakikisha Katiba na Kanuni zinafuatwa na Kulindwa.

12.1.9    Kumwajiri Mratibu na watumishi wengine wa viwawa.

12.1.10Kuitisha mikutano kwa mujibu wa Katiba.

12.1.11Kutoa Taarifa za Utendaji katika mikutano.

12.1.12Kumsimamisha kiongozi,waajiriwa walioshindwa kutekeleza majukumu na maadili ya chama.

12.1.13Kuhudhuria vikao, mikutano, warsha, makongamano, ndani na nje ya chama.

12.1.14Kupokea, kujadili na kuthibitisha taarifa za kamati ndogondogo.

 

12.2Majukumu ya Halmashauri ya Utekelezaji (Kigango, Parokia, Jimbo, Taifa)

12.2.1    Kupokea, kujadili na kupitisha taarifa za utekelezaji kutoka kwenye kamati tendaji na kuziwasilisha katika mkutano mkuu.

12.2.2    Kupokea na kujadili hatua za kinidhamu zilivyopendekezwa na Kamati Tendaji ili kuidhinisha na kutoa mapendekezo kwa ajili ya kuwasilishwa kwenye mkutano mkuu.

 

12. 3 Majukumu ya Mkutano Mkuu (Kigango, Parokia, Jimbo na Taifa)

12.3.1  Ni kikao cha juu kuliko vyote ya maamuzi ya mwisho  kuhusu mambo yote ya VIWAWA.

12.3.2  Kupokea na kujadili taarifa ya Halmashauri ya utekelezaji

12.3.3  Kuchagua Viongozi wa Kamati Tendaji.

12.3.4  Kujadili na kupitisha makisio na ripoti ya mapato na matumizi ya viwawa

12.3.5  Kuweka Maazimio.

12.3.6  Kuchunguza Muundo wa Chama.

12.3.7  Kupitisha marekebisho ya Katiba (ngazi ya Taifa).

12.3.8  Kuchukua hatua za kinidhamu ikiwa ni pamoja na kumvua madaraka Kiongozi          yeyote wa viwawa au kufuta uanachama wa mwanachama yeyote.

12.3.9  Kurekebisha, kusahihisha, kubatilisha uamuzi wowote uliotolewa na vyombo vya chini yake.

 

13.0   MAPATO YA CHAMA.

13.1     Vyanzo vya mapato

 

13.1.1  Ada ya Uanachama. Kila Parokia na Jimbo linapaswa kulipa ada kwa kiwango kilichokubaliwa kwa mwaka ili kuchangia uendeshaji wa shughuli za viwawa katika ngazi zote. 

13.1.2    Washirika wahisani kutoka sehemu mbalimbali.

13.1.3    Shughuli za kutunisha mfuko

13.1.4  Miradi mbalimbali ya VIWAWA.

 

13.2      Uwekaji wa fedha

13.2.1    Fedha ni Lazima ziwekwe Benki kwa jina la Chama.

 

13.3      Utoaji wa fedha

13.3.1    Ni lazima uwe na jina na sahihi ya mweka hazina, mwenyekiti pamoja na mshauri wa chama.

13.3.2    Matumizi yote yapate kibali cha kamati ya utendaji na mshauri.

 

13.4      Ukaguzi wa fedha    

   Vitabu vya fedha na mali zote za chama zitakaguliwa kama ifuatavyo:

 

   13.4.1 Taifa    -  Mkaguzi kutoka Taifa.

   13.4.2 Jimbo   -  Mkaguzi wa Jimbo

   13.4.3 Parokia -  Mkaguzi wa Parokia

 

14.0   KAMATI NDOGO NDOGO

 

Kamati ndogondogo zinaweza kuundwa kadiri ya mahitaji. Zifuatazo ni lazima ziwepo katika kamati tendaji.

 

14.1     Kamati ya Litrujia, Elimu na Mafunzo.

14.2     Kamati ya Michezo, Burudani na Mahusiano.

14.3     Kamati ya Uchumi, Mipango na Fedha .

 


14.4 Wajumbe wa Kamati:(ndogondogo)


 

Wajumbe wa kamati huteuliwa na Kamati Tendaji kwa kuzingatia karama ya utume  waliyonayo katika kamati husika na uwajibikaji wake katika shughuli za kujitolea kwa kumtangaza Kristu kupitia karama alizozawadiwa na Mungu, wajumbe wanne kutoka Halmashauri husika. Viongozi wa Kamati Tendaji watakuwa wajumbe katika kamati hizo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

14.5     Majukumu ya kamati ya Uchumi, Mipango na Fedha

 

14.5.1  Kuangalia na kusimamia miradi ya Viwawa katika ngazi husika.

14.5.2  Kubuni mbinu mpya ya kupata fedha za kuendesha shughuli za chama, na kutoa ushauri wa kitaalamu juu ya namna ya kutunza hesabu.

14.5.3  Kubuni miradi mbalimbali, kupendekeza bajeti ya chama na kubuni mbinu za kudhibiti matumizi.

14.5.4  Kutoa taarifa ya maandishi kuhusu mapendekezo ya vikao vya Kamati kwa Kamati Tendaji, watakutana mara 1 kwa mwezi na kwa dharula.

14.5.5  Kuhakikisha kila mjumbe wa kamati anapata haki ya kutoa mapendekezo na ushauri ndani ya vikao.

14.5.6  Kushirikiana na  Kamati Tendaji na kamati zingine ndogondogo ili kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu yaliyopo kwa wakati huo.

14.5.7   Kushirikiana na mhazini katika kutengeneza repoti ya fedha ya mwaka.

 

            14.6     Majukumu ya kamati ya Litrujia, Elimu na Mafunzo


 

14.6.1 Kusimamia ibada za misa za vijana na kuhakikisha huduma za Misa zimeandaliwa na kutoa taratibu za Misa.

14.6.2  Kusimamia malezi ya wanachama kwa njia za mafundisho mbalimbali kama Biblia Takatifu, Tafakari ya Maisha.

14.6.3  Kuongoza na kuratibu ufundishaji wa sala na tafakari ya Neno la Mungu na ibada mbalimbali zinazoongozwa na Viwawa.

14.6.4  Kuandaa Semina, Mafungo, Matendo ya Huruma, Hija,Kongamano kwa vijana.

14.6.5  Kuhakikisha kila mjumbe wa kamati anapata haki ya kutoa mapendekezo na ushauri ndani ya vikao.

14.6.6  Kutoa taarifa ya maandishi kuhusu mapendekezo ya vikao vya kamati kwa Kamati Tendaji, na watakutana mara moja kwa mwezi na kwa dharura.

14.6.7  Kushirikiana na na Kamati ya Utendaji. Kamati zingine ndogondogo ili kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu yaliyopo kwa wakati huo.

 

14.7 Majukumu ya Kamati ya Michezo, Burudani na Mahusiano


 

14.7.1 Kusimamia michezo na kupanga michezo mbalimbali ya chama kama mpira wa

miguu,mpira wa kikapu,mpira wa pete.

14.7.2  Kuandaa michezo na mashindano mbalimbali kwa kushirikiana na viongozi wa  Kamati Tendaji.

14.7.3  Kuanzisha timu za michezo ya nje mfano mpira wa miguu, kikapu, na pete

14.7.4  Kuandaa michezo ya kuigiza mfano Mateso ya Yesu, Fatima, Bakhita na mingine itakayojitokeza.

14.7.5  Kuanzisha vikundi vya utamadunisho mfano ngoma, Ngonjera, Jaiving, nyimbo.

14.7.6  Kuandaa na kuratibu sherehe na burudani mbalimbali ambazo chama zitakuwa nazo katika kipindi cha mwaka mfano pikiniki, sherehe.

14.7.7  Kutoa taarifa za maandishi kuhusu mapendekezo ya vikao vya kamati kwa Kamati Tendaji, watakutana mara moja kwa mwezi na kwa dharula.

14.7.8  Kuhakikisha kila mjumbe wa kamati anapata haki ya kutoa mapendekezo na ushauri ndani ya vikao.

14.7.9  Kushirikiana na Kamati ya Utendaji.Kamati zingine ndogondogo ili kuleta ufanisi katika kutekeleza majukumu yaliyopo kwa wakati huo.

 

 

 

 

 

 

8 comments:

  1. Asante sana kwa Elimu mungu akubariki

    ReplyDelete
  2. Pdf please tunahitaji ni mhimu kwa vijana

    ReplyDelete
  3. Asante Swali langu je kiongoz ngazi kuu viwawa kamat tendaji akiwajibishwa kwa mujibu wa kanuni kwa utovu wanidham ikiwepo utatatishaji fedha za vijana anaruhusiwa kuchaguliwa tena kuwa kiongoz kandaa??

    ReplyDelete
  4. Mapendooooo, sioni sehemu ya ku download pdffff

    ReplyDelete
  5. Mnaweza nitumia whatsapp 0623056162

    ReplyDelete
  6. Me pia sioni sehemu ya kudownload kama mnawez naomb mtumie kwa whatsap namba 0754929091

    ReplyDelete