Kuhusu viwawa


USHIRIKA WA VIWAWA NI NINI?
Viwawa ni ushirika mkubwa wa vijana ambao kwa matendo na tafakari hujaribu kubadii na kukuza/kustawisha maisha yao nay a jamii.
 VIWAWA: ni chama cha kitume cha Vijana Wakatoliki Wafanyakazi ambao wanatumwa na Kanisa ili neza habari njema ya kwamba Yesu Kristu ndiye njia ya ukweli na uzima kwa vijana wote katika maisha yao ya kila siku. 
Wafanyakazi: Ni vijana wa wanaume na wanawake waishio mijini, vijijini na walio kwenye masomo, mafunzo ya fani mbalimbali, walio katika ajira rasmi na zisizo rasmi. 

Viwawa ni chama ambacho kinawaunganisha vijana na kuwasaidia waone hali yao, kuamua juu yake katika mwanga wa Injili na kuwaongoza kufanya matendo ya kubadilisha hali zao na kutengeneza ziwe nzuri zaidi kwa njia ya Tafakari ya Maisha.
Chama hiki huongozwa na vijana wenyewe katika ngazi zote na huwa na Mshauri na Mlezi kwa ngazi ya Parokia,Jimbo na Taifa.Soma zaidi katiba ya viwawa Tanzania

NANI ANAENDESHA VIWAWA?
Viwawa inaendeshwa katika ngazi ya jumuiya, vigango, parokia,majimbo taifa na kimataifa na vijana wenye umri kati ya miaka 14 mpaka 35. Vijana  huamua mambo ya kufanya baada ya kutathimini uhalisi wa mazingira, pamoja na hali ya watu wanaowazunguka.

VIWAWA INAFANYA SHUGHULI GANI?
Viwawa huwakusanya vijana pamoja na kuwasaidia kupata majibu ya mahitaji yao na mahitaji ya vijana wengine kupitia matendo.matendo haya huamuliwa katika vikundi kupitia majadiliano yajulikanayo kama DODOSO(njia ya kushirikishana matatizo na changamoto zinazowakabili)
Matendo yanaweza kufanywa na mwanachama mmojammoja kwa kuwasaidia marafiki kutatua matatizo katika kazi zao, familia na mahusiano. Matendo ya viwawa pia hufanywa na vijana kwa pamoja katika vikundi.
Mfano:
·         Kufanya kampeni juu ya haki za vijana
·         Kufanya kazi ili kupata zana bora
·         Kuandaa matukio ya kuwasaidia vijana wasiojiweza
Kwa njia hii viwawa inaweza kusaidia maendeleo ya jumuiya.

KITU GANI KIZURI ZAIDI KUHUSU VIWAWA?
Zaidi ya ukweli kuwa viwawa inaendeshwa na vijana wenyewe, inasababu nyingine tatu muhimu za kuwepo.
1.      Ni nafasi ya kuitumia kuchukua hatua kuboresha jamii ndogondogo na jamii kubwa
2.      Viwawa wanasaidia kujenga ujasiri, ujuzi binafsi, imani, kujitambua kwa vijana.
3.      Viwawa wanasaidia vijana kukutana na marafiki wapya nchini kote na hata duniani kote kupitia matendo yao, mikutano katika mafunzo, likizo na mikusanyiko mbalimbali.viwawa ni uzoefu wa thamani inayofurahisha.

   VIWAWA ILIANZAJE?
Viwawa ilianzishwa Ubelgiji mwaka wa 1925 katika jumuiya ya wafanyakazi waliokuwa wakiishi nje kidogo na mji wa Brussels na Padri kijana aliyeitwa Joseph Cardijin.Padre Cardjin alijihisi kutengwa na marafiki zake kwa kuamua kuwa padre na alikuwa anaguswa na jinsi ya wafanyakazi walivyokuwa wanawekwa mbali na kanisa.Aliamini kuwa ujumbe wa Yesu ulikuwa kwa ajili ya wafanyakazi na maskini, na hivyo alijitoa katika kuwaunganisha kwa ajili ya kazi ya tafakari ya Injili na matendo ya jamii.


KWA JINSI GANI USHIRIKA WA VIWAWA UNA UMUHIMU LEO?
Viwawa inapatikana katika nchi zaidi ya 100 ulimwenguni kote na ina wanachama zaidi ya milioni 3. Kwa zaidi ya miaka 70 iliyopita, viwawa ilikuwa na msukumo endelevu wa mabadiliko kama ambavyo imekuwa ikipanuka ulimwenguni kote.

NITAJIUNGAJE NA VIWAWA?
Kuna vikundi vidogo vidogo katika ngazi ya Parokia nchini  kote. Vikundi hivyo hukutana mara kwa mara kupanga mambo ili kuwahudumia, kuwaelimisha na kuwawakilisha vijana. Ili uweze kujinunga wasiliana na viwawa kwa kutumia anuani iliyoko nyuma ya kipeperushi hiki na watakueleza wapi kikundi cha karibu kinapatikana.
 Vinginevyo waweza kumuuliza Paroko wa Parokia yako au kiongozi wa kanisa. Hakika viwawa ni uzoefu wa thamani inayofurahisha.

NINAHITAJI KUCHANGIA FEDHA?
Ndio, kila kijana hulipa kiasi kidogo cha ada kwa viwawa kwa ajili ya kujiunga pamoja na michango ya kikundi Parokiani.Kwa kupitia uwajibikaji huu, wanachama watajishughulisha na hivyo kumiliki ushirika wao wenyewe.

VIWAWA NI KWA AJILI YA NANI?

Ni kwa ajili ya kila mmoja.Kila kijana mwenye umri kati ya miaka 14 hadi 35 anaweza kuwa mwanachama. Wale wenye umri  wa miaka 14 -17 huwekwa pamoja( hawa ni wale ambao bado wanasoma muda wote au wanasoma kwa muda mfupi katika ufundi stadi). Uanachama wa kudumu kwa miaka 18 na kuendelea uko wazi kwa waliomaliza masomo, wafanyakazi wakudumu au wa muda, wazazi au wanaotafuta kazi.viwawa inahusika kwa namna ya pekee na kundi la vijana wafanyakazi katika jamii ya kisasa.


USHIRIKA HUU UNAENDESHWAJE?
Viwawa ina ngazi mbalimbali katika uendeshaji, ngazi ya mwanzo nay a muhimu ni ngazi Jumuiya, Kufuatiwa na vigango na Parokia na hujumuisha vijana ambao hukutana jumuiyani pamoja na kuchagua viongozi wao, huchangia mfuko wao wa fedha na kuamua matendo kulingana na mahitaji yanayowazunguka. Viwawa  pia ina ngazi za jimbo, taifa na kimataifa ili kusaidia na kukuza kazi za jumuiya,vigango na parokia.wawakilishi wao waliochaguliwa hupeleka maoni katika ngazi hizi na husaidia katika malezi na mafunzo ya uongozi wa shirika.

KWA NINI VIWAWA INAITWA SHULE YA MAISHA?
Viwawa ni shule ya maisha kwa sababu sio tu huzungazitia vijana wa leo bali pia hukuza ujuzi wao wa kuwasiliana na kujiendesha ambao huwafaa kama viongozi. Malezi yao haya huzaa viongozi sio tu kwa ajili ya ushirika huu lakini pia kwa maisha yote.Hivyo hutoa mchango ulio wazi katika kanisa na katika jamii.

NI KWA VIPI VIWAWA NI USHIRIKA WA KIKRISTU?
Viwawa inaongozwa na mafundisho ya Kristo, kazi yake inaongozwa na tafakari ya Injili ambayo huwa ndiyo utangulizi msingi wa kila mkutano. Hii huthibitisha hadhi na lengo ambavyo Mungu amempatia kila kijana kwa maisha.Misingi ya mwanzo ya ushirika huu ni Padre Cardjin na Kanisa Katoliki; vile vile hutafuta namna ya kushirikishana na madhehebu mengine, ukiamini kuwa taratibu na malengo yake yatapokelewa na madhehebu yote.

JE WATU WAZIMA HUSHIRIKI KATIKA VIWAWA?
Ndio, zaidi ya viongozi wa kuchaguliwa katika jumuiya, pia kuna mlezi/mshauri. Kwa kawaida huwa ni Padre ingawaje hata sasa anaweza kuwa Mlei, Mtawa,au Katekista.Kazi ya Mlezi/Mshauri ni muhimu sana kwa malezi ya vijana, lakini hasa katika kuwaunga mkono na kuwasaidia na si katika kuongoza.

Ushirika huu una muundo wake wa kujitegemeza na hutoa mafunzo kwa ajili ya walezi/washauri wake.

10 comments: