Tafakari

Ee YESU UNISAIDIE NIWEZE KUKUFUATA KWA MOYO WOTE-AMINA: "BASI MTIINI MUNGU"
NENO LA HEKIMA:
SALA YA SIKU:
Anza kufanya yaliyo ya muhimu. Kisha fanya yale yanayowezekana. Na mara utakuwa unafanya yale Yasiyowezekana.. Kutoka kwa Mt. Fransisco wa Asis
 
 
.
Kristo Yesu. tuwezeshe kuwa na moyo imari, tuwe na imani thabiti kwako.Bwana Mfufuka, umeleta kwetu mwanga wa msamaha wako,Hiyo ni zawadi kamilifu, na kwa kila mtu kuthubutu kuamsha furaha ya Mungu kwetu
 
.
INJILI YA LEO MATHAYO 11:20-24 :
 Ndipo akaanza kuikemea miji ile ambamo ndani yake ilifanyika miujiza yake iliyo mingi, kwa sababu haikutubu. Ole wako, Korazini! Ole wako, Bethsaida! Kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Tiro na Sidoni, wangalitubu zamani kwa kuvaa magunia na majivu.
Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi Tiro na Sidoni kustahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi. Nawe Kapernaumu, je! Utakuzwa mpaka mbinguni? Utashushwa mpaka kuzimu; kwa kuwa kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika katika Sodoma, ungalikuwapo mji huo hata leo.
Walakini nawaambieni, itakuwa rahisi nchi ya Sodoma kustahimili adhabu yake siku ya hukumu kuliko wewe

Swali la kusaidia tafakari binafsi ya Injili hii:
Ni kwa jinsi gani ninaiweka nafsi yangu mbele ya Habari njema ya Yesu kristo? Kama Yohane Mbatizaji, au kama watu wenye nia,kama madactari au kama watu masikini?
SOMO LETU LA BIBLIA:(TAFAKARI YETU)2.Kor 4:2-6 
Lakini tumekataa mambo ya aibu yaliyositirika, wala hatuenendi kwa hila, wala kulichanganya neno la Mungu na uongo; bali kwa kuidhihirisha iliyo kweli twajionyesha kuwa na haki, dhamiri za watu zikitushuhudia mbele za Mungu.
Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea;
ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.
Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali Kristo Yesu ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe kuwa tu watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang'aa toka gizani, ndiye aliyeng'aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo. 

Maswali ya Tafakari Binafsi:
  1. Je! sisi ni watumishi wa Yesu kristo? Ni kwa namna gani tunawatumikia wengine kwa ajili ya kristo?
  2. Je! mimi ninaenenda katika haki? Kwa namna gani ninaliishi Neno la Mungu?
  3. Ni mambo gani ya aibu tunayopaswa kuyakataa?
  4. Je nina nuru elimu ya utukufu wa Mungu moyoni mwangu?
NB: Karibu tutafakari andiko hili:

2 comments:

  1. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by a blog administrator.

    ReplyDelete